• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Seneti Yapinga KDF Kupewa Mamlaka Ya Kusimamia KMC.

    (GMT+08:00) 2020-09-21 16:41:02

    Maseneta nchini Kenya wamepinga hatua ya serikali kuhamisha usimamizi wa Kiwanda cha kutayarisha Nyama Nchini (KMC) kutoka Wizara ya Kilimo hadi ile ya Ulinzi wakisema hatua hiyo ni kinyume cha Katiba.

    Wakichangia hoja kuhusu suala hilo Alhamisi, walisema hatua hiyo ni haramu kwa sababu uamuzi huo ulifikiwa bila kushirikishwa kwa umma katika mpango huo, ikizingatiwa kuwa KMC ni asasi ya serikali iliyobuniwa kutokana na sheria iliyotungwa na bunge.

    Huku wakilaani kile walichotaja kama hatua ya Rais Kenyatta kuweka usimamizi wa asasi za umma chini ya wanajeshi, maseneta hao wamewataka mawaziri Peter Munya (Kilimo) na Monica Juma (Ulinzi) kufika mbele yao kuelezea sababu zilichangia kuhamishwa kwa KMC hadi jeshi (KDF). KMC ilhamishwa hadi KDF wiki moja iliyopita kupitia amri ya Rais Kenyatta. Amri hiyo iliwasilishwa na Waziri Munya kwa Katibu wa Idara ya Uvuvi Harry Kimtai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako