Nchi ya Ethiopia ikikaribisha Noti Mpya, Waziri Mkuu Abiy Ahmed ametangaza kutolewa kwa noti mpya za birr katika juhudi za kupambana na ufisadi.
Noti mpya za birr 10, 50 na 100 zilitolewa mwanzoni mwaka wiki, pamoja na kuletwa kwa mara ya kwanza kwa noti ya birr 200.
Kulingana na waziri mkuu, Ethiopia inaondoa noti za zamani ili kukabiliana na "ufisadi, ubadhirifu na biashara haramu", na hivyo kuchochea zaidi uchumi ulioathiriwa na sababu ikiwa ni pamoja na janga la Covid-19.
Noti mpya itanza kutumika na zile ya zamani zitaondolewa ndani ya miezi mitatu.
Kwa hivyo Waethiopia lazima wabadilishe noti za zamani na zile mpya katika benki kote nchini.
Muundo wa noti mpya utafanya vigumu kwa utengenezaji wa noti bandi.
Kupitia Noti mpya Uchumi wa Ethiopia utaongeza kwani benki zitapata nafasi ya kukusanya pesa nyingi.
Hata kama serikali inaweza kuwa na sababu kadhaa za kubadilisha noti, hatua hiyo ya hivi karibuni itakuwa na jukumu muhimu katika kukusanya pesa zote ambazo zimefichwa manyumbani au ofisini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |