• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Mashariki Uzalisha wa maua umesalia chini

    (GMT+08:00) 2020-09-22 19:21:35

    Uzalisha wa maua umesalia chini hata wakati msimu mkuu wa soko la kuuza nje la Kenya unapoanza, hali ambayo imeona mashamba makubwa yakishindwa kutimiza mahitaji ya soko la nje.

    Uzalishaji wa kilimo cha maua na mboga, umebaki chini tangu Aprili wakati athari za Covid-19 nchini zilizidi kuwa mbaya, na kuathiri vibaya mavuno.

    Oserian, shamba kubwa zaidi la maua nchini Kenya, limesema haliwezi timiza mahitaji ya wateja wao kutoka nje kwa sababu ya uzalishaji mdogo.

    Uzalishaji wa maua katika miezi nane iliyopita ulipungua kwa asilimia 20 huku mboga ikipungua kwa asilimia 23, ikionyesha athari ambayo coronavirus imekuwa nayo kwenye tasnia.

    Takwimu za tasnia kutoka kwa mdhibiti zinaonyesha kuwa ujazo umeshuka hadi kilo milioni 211 katika kipindi cha ukaguzi kutoka milioni 230 katika kipindi kinachofanana cha 2019.

    Sekta hiyo iliathirika vibaya baada ya kusitizwa kwa maagizo huko Uropa, ambayo yaliona mashamba ya maua yakipunguza uzalishaji ili kuepusha hasara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako