Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetengeneza zaidi ya viwango 100 ambavyo vitatumika kudhibiti ubora katika sekta ya madini kwenye masuala ya utafiti, uchimbaji na uchenjuaji.
Akizungumza katika maonyesho ya tatu ya madini na teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya Magogo mkoani Geita, msemaji wa TBS, Roida Andusamile alisema kuwa viwango hivyo vimeandaliwa kudhibiti viwango kwa wachimbaji wakubwa na wadogo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |