SIKU chache baada ya serikali za Tanzania na Uganda kukubaliana juu ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima hadi Chongoleani, Tanga, Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) limesema litatangaza upya zabuni ya utekelezaji wa mradi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk. James Mataragio, amesema kuna vikwazo vilijitokeza baada ya mradi kusimamishwa ambapo kuna kampuni zilikuwa tayari zimeshinda zabuni na zilikuwa kwenye hatua ya kukamilisha mchakato wa manunuzi.
Alibainisha kuwa kampuni zilizokuwa zimeomba zitarekebisha vitu mbalimbali kutokana na gharama nyingine zimepanda na kushuka, na hivyo hatua hiyo itachelewesha kidogo mchakato wa manunuzi.
Hata hivyo, alisema kutokana na mkataba huo wa awali kusainiwa kuna mkataba hodhi ambao utasainiwa na wawekezaji na kuna mikataba mingine midogo midogo ambayo itakamilishwa Desemba mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |