• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: wadau wa kilimo wazitaka benki kuondoa masharti ya mikopo

    (GMT+08:00) 2020-09-23 18:57:37

    Taasisi zinazojihusisha na masuala ya kuhamasisha kilimo nchini, zimeiomba serikali kuboresha na kuondoa baadhi ya masharti yaliyowekwa na taasisi za kifedha ili kuwasaidia wakulima kukopesheka kwa urahisi.

    Ofisa Masoko wa Kampuni ya Agricom kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Peter Mwita, amesema kilimo ni miongoni mwa sekta zilizochangia kwa kiasi kikubwa nchi kufikia uchumi wa kati na kuhakikisha mkulima anakuwa sehemu ya mafanikio hayo lazima mazingira wezeshi yaandaliwe.

    Alisema miongoni mwa mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi ni serikali kuziangalia au kuzishauri taasisi za kifedha kuwaandalia mazingira rafiki ya ukopeshaji ili yasimuumize mkulima na aweze kurejesha kwa wakati.

    Aliongeza kuwa kampuni ya Agricom ambayo inahusika na uuzaji pamoja na usambazaji wa zana za kilimo imekuwa mstari wa mbele kujali hali za wakulima kwa kuhakikisha wanauza zana zao kwa bei nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako