Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Madini ,petrol na gesi nchini Rwanda (RMB) , Francis Gatare, amesema kuna matumaini kwamba sekta ya madini ya nchi hiyo itafufuka hivi karibuni kutokana na athari zilizoletwa na janga la Covid.
Sekta ya madini ya Rwanda,kama zilivyo sekta nyingine duniani,imeathiriwa pakubwa na janga la korona,haswa kutokana nan chi kufungwa katikati ya mwezi Machi,na kusitisha shughuli zote.
Fauka ya hayo,sekta hiyo imeathiriwa na kushuka kwa bei za kimataifa za madini kutokana na ununuzi mdogo uliosababishwa na janga la Covid-19.
Nchini Rwanda uchimbaji wa madini ya cassiterite,wolfram (tungsten),na coltan uliathirika kwa kiwango kikubwa,madini ambayo yamefanya nchi hiyo kuorodheshwa miongoni mwa wazalishaji wakuu duniani.
Takwimu zinaonyesha kuwa mapato ya mauzo ya nje ya madini hayo yalipungua kwa asilimia 30.9 mwezi Januari na Februari 2020 ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka jana.
Hata hivyo ,kulingana na Gatare,urejeaji mapeama wa shughuli za uchimbaji madini umefufua matumaini kwamba sekta itaimarika hivi karibuni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |