Wachimbaji wadogo wa madini mkoani Mbeya nchini Tanzania, wamesema wanalazimika kukopa fedha kwa watu binafsi na taasisi zisizokuwa rasmi kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zao kutokana na kukataliwa na taasisi rasmi kwa madai kuwa hawana vigezo vya kukopesheka.
Waliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya mikopo ya vitendea kazi vya kuchimbia madini kwa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa kutoka katika mikoa ya Mbeya na Songwe yaliyoandaliwa na benki ya NMB.
Mmoja wa wachimbaji hao, Aidan Msigwa, mchimbaji mdogo wa dhahabu katika Wilaya ya Chunya, alisema pamoja na wakopeshaji binafsi riba yao ni kubwa, lakini hawana masharti magumu kama benki.
Alisema yeye ni mmoja wa watu walioumizwa na mikopo ya wakopeshaji binafsi kwa madai kuwa alienda kuomba mkopo kwenye moja ya benki ambayo ilimnyima na hivyo kuamua kwenda kukopa kwa mtu binafsi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |