Wakati mafuriko yakiendelea kuathiri taifa la Uganda, Shirika la Chakula na Kilimo (FAO),limeonya kuhusu uwezekano wa ukame mkali kati ya Novemba hadi Februari 2021 ambao utasababisha uhaba wa chakula nchini.
Onyo hili lilitolewa huko Kampala wakati wa makabidhiano ya pikipiki 190 na FAO kwa Serikali za mitaa 29 katika korido ya ng'ombe, West Nile na eneo dogo la Karamoja.
Mwakilishi wa FAO nchini Uganda Antonio Querido, alisema wafanyakazi wa kilimo katika Wilaya 29 watatumia pikipiki hizo kuwafikia wakulima na kuongeza uelewa juu ya hatua za mabadiliko ya hali ya hewa kama vile kupanda miti na uhifadhi wa maji.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |