Tanzania na Afrika Kusini zimeunda kamati ya pamoja yenye wajumbe kutoka nchi hizo, ili kushirikiana katika kutekeleza hati ya makubaliano(MoU) kwenye masuala ya viwanda, biashara na uwekezaji.
Hatua hiyo ilifikiwa mwishoni mwa wiki jana jijini Dodoma, katika kikao cha pamoja kati ya Kaimu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashar, Ally Gugu, na ujumbe kutoka Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania.
Akizungumza na ujumbe huo, Gugu alisema nchi hizi mbili zimekuwa na ushirikiano wa kibiashara, kiuchumi na kisiasa kwa muda mrefu tangu kipindi cha kudai uhuru.
Aliongeza kuwa lengo la hati hiyo ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara zaidi kwa kuongeza biashara kwa maslahi ya pande zote mbili, hasa ikizingatiwa Afrika kusini ni moja ya nchi vinara katika uwekezaji barani Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |