• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WAHASIBU AFRIKA MASHARIKI WAJIPANGA KUFUFUA UCHUMI BAADA YA CORONA.

    (GMT+08:00) 2020-09-28 18:31:47

    Wahasibu waandamizi wamezitaka nchi za Afrika Mashariki kuweka mikakati kadhaa ili kufufua uchumi wan chi zao ulioathirika kutokana na athari za virusi vya corona. Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa ACCA Tanznaia, Jenard Lazaro mwishoni mwa wiki jana, wakati wa mkutano wa Chama cha Wahasibu Ulimwenguni (The Association of Chartered Certified Accountants-ACCA)

    Akizungumza katika mkutano huo, ulioandaliwa kwa kushirikiana na Bodi za Wahasibu za nchi za Afrika Masharik, pamoja na bodi ya taifa ya wahasibu na wakaguzi wa Hesbau (NBBA), Tanzania, alisema nchi za Afrika Mashariki hazina budi kujifunza kutokana na changamoto zilizojitokeza wakati wa mapambano ya janga la virusi vya corona.

    Alisema NBBA imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika kufanikisha malengo ya mkutano huo hasa katika kuangalia athari za virusi vya corona katika biashara na fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako