Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuuza nje bidhaa nchini Kenya (KEPROBA) Wilfred Marube, amesema Kenya imepanga kuzingatia soko la China ili kuongeza mauzo yake katika miaka michache ijayo.
Marube amesema China inatoa uwezo mkubwa zaidi kati ya washirika wa sasa wa biashara wa nchi hiyo kwa sababu ya idadi kubwa ya watu na nguvu kubwa ya ununuzi.
Amesema shirika hilo la kuuza nje litaunda uwezo kwa kampuni za Kenya kutimiza mahitaji ya kufikia soko la China.
Kulingana na KEPROBA, parachichi za Kenya tayari zimepata soko la China na bidhaa zingine kadhaa zitaanza kuuuzwa hivi karibuni.
Amesema pia Kenya inatafuta bidhaa zingine ambazo sio za kilimo ambazo zitavutia watumiaji wa China ili kupanua zaidi soko.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |