Shirika la ndege la Ethiopia limeendelea kuhimili makali ya janga la corona na kipindi kigumu cha biashara na linatarajia kuanza kurejea hali ya kawaida mapema iwezekanavyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Tewolde Gebremariam amesema limepoteza zaidi dola bilioni 1 wakati wa janga la corona lakini hadi sasa limeweza kuzuia kutafuta uokoaji au kufutwa kazi kwa wafanyikazi wake.
Lilipata faida ya dola milioni 44 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2020.
Shirika hilo ambalo ni kubwa zaidi barani Afrika,hadi sasa limefanya safari 360 kusafirisha vifaa vya kujikinga na corona kwa zaidi ya nchi 80.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |