• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waendeshaji magari watalipa Sh3,000 zaidi  kupitia bima yao ya kila mwaka ya gari

    (GMT+08:00) 2020-09-30 19:07:21

    Waendeshaji magari watalipa Sh3,000 zaidi kupitia bima yao ya kila mwaka ya gari ili kulipia uharibifu wa mali za barabarani ikiwa marekebisho ya sheria yatapitishwa.

    Bodi ya Barabara ya Kenya (KRB) inataka kutenga kati ya Sh500 na Sh3,000 kutoka kwa bima ya kila mwaka ya mtu mwingine itakayotumika kuchukua nafasi ya miundombinu ya barabara iliyoharibiwa kama alama, vituo vya usalama na taa za barabarani wakati wa ajali.

    Kiasi kitatofautiana kulingana na uwezo wa injini ya gari na mpango huu uantarajiwa kuzalisha zaidi ya Sh10 bilioni kila mwaka.

    Kaimu mkurugenzi mtendaji wa KRB Rashid Mohamed amesema kuwa hatua hiyo itahitaji marekebisho ya Sheria ya Bima ili kuondoa fidia ya mali za barabara kutoka kwa mtu mwingine na kuingiza ada.

    Ada hizo zitapelekwa kwa KRB.

    Aidha amesema tayari mali zilizoharibiwa, iwe ni kutokana na ajali au viti vyengine tayari zimegharamiwa na Sh18 kwa lita ya mafuta waendesha magari wanalipa wakati wa kununua mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako