Shirikishio la Soka Tanzania (TFF), limesaini mkataba wa kudumu na Chama cha Maendeleo ya Michezo cha Malya kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa mchezo huo nchini Tanzania. Halfa ya kusaini mkataba huo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Kituo cha Maendeleo ya Michezo cha Dar es Salaam. Mwenyekiti wa TFF Bw. Wallace Karia, amesema mkataba huo utasaidia kupeleka wataalamu wao kujifunza mbinu za kusimamia vyema maendeleo ya michezo mbalimbali . Amesema hiyo ilikuwa ni moja ya sera zake wakati anaingia madarakani kuhakikisha Tanzania inakuwa na Chuo cha Michezo ili kuwaandaa viongozi waadilifu na kila idara inakuwa na viongozi wenye weledi. Kiongozi huyo amewataka wasemaji wa klabu mbalimbali hapa nchini kushiriki kozi inayohusiana na kazi wanayoifanya ili wafahamu vyema namna ya kutekeleza majukumu yao na kuacha kuepuka porojo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |