Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Neymar da Silva Santos Junior anatajwa kuwa na deni la Sh4.4 bilioni za mamlaka ya kodi nchini Hispania. Tovuti ya Get French News imesema mamlaka hiyo imetoa orodha ya watu binafsi na kampuni inazowadai fedha. Katika orodha hiyo, kuna mshambuliaji wa Brazil na PSG, Neymar, ambaye anatakiwa kulipa kodi ya Euro 34.6 milioni. Kiasi hicho cha fedha, kinaendana na kodi ambayo Neymar hajalipa kutokana na marupurupu aliyopokea kutoka kwa waajiri wake wa zamani Barcelona alipokuwa ameongeza mkataba mwaka 2016 kabla ya kuhamia mjini Paris nchini Ufaransa mwaka 2017 akiwa hajakamilisha mkataba wake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |