Bei ya maziwa nchini Kenya inatarajiwa kupanda kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo kwenye soko. Katibu mkuu wa wizara ya mifugo nchini Kenya Bw Harry Kimutai amesema hali hiyo imetokana na kupungua kwa bidhaa hiyo kwenye soko na wakulima kutaka malipo ya juu. Kwa mujibu wa Bw Kimutai, nusu lita ya maziwa sasa itakuwa ikiuzwa shilingi 46 kutoka 43, ikiwa ni ongezeko la kwanza kwa bidhaa hiyo tangu mwaka wa 2018. Bidhaa nyingine ambazo zinatokana na maziwa pia zinatarajiwa kuongezwa bei. Bodi ya maziwa nchini Kenya imesema idadi ya lita za maziwa wanazoletewa na wakulima zimepungua kutoka lita milioni 60 katika mwqezi wa Januari hadi lita milioni 43 katika mwezi wa Juni. Hivi sasa kampuni nyingi za maziwa zinapitia kipindi kigumu kutokana na kupungua kwa idadi ya lita wanazopokea kutoka kwa wafugaji.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |