Serikali ya Uganda imewataka watu wanaojihusisha na uzalishaji wa kahawa nchini humo kukumbatia usindikaji kwa ajili ya kuvutia soko la kimataifa. Kwa mujibu wa katibu mkuu mtendaji wa mamlaka ya kahawa nchini Uganda Emmanuel Lyamulemye ili wafanya biashara wanaojihusisha na kahawa wafaidike basi watahitajika kutengeneza kahawa yenye ubora na kukumbatia usindikaji hali ambayo itaimarisha soko la kahawa nchini humo.
Ameongeza kuwa serikali ya Uganda hivi sasa inaendelea kuhimiza ubora kwenye uzalishaji wa kahawa ili kuvutia soko la kimataifa.
Ameongeza kuwa soko la kahawa kote duniani limeathiriwa na janga la corona lakini akawataka Waganda kujifunza ili changamoto kama hiyo isiwakumbe katika siku zijazo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |