Mikopo ya Fuliza katika miezi sita iliongezeka na kufikia Sh176 bilioni kutoka Sh81 bilioni katika kipindi kama hicho mwaka uliopita, ikionyesha kukopwa kwa Sh967 milioni kila siku.
Fuliza inafadhiliwa na benki ya KCB na NCBA , ambayo tayari zilikuwa na ushirikiano na Safaricom kutoa mikopo ya muda mfupi kwenye jukwaa la M-Pesa.
NCBA imesema ilikopesha Sh132 bilioni kupitia Fuliza katika miezi sita hadi Juni wakati KCB ilitoa mikopo yenye thamani ya Sh44 bilioni.
Fuliza inaruhusu wateja kumaliza shughuli za M-Pesa wakati hawana pesa za kutosha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |