Biashara ndogo na za kati nchini Uganda hazifai kuchukua mikopo ili kuwekeza katika sekta ya mafuta na gesi.
Haya ni kwa mujibu wa Shirikisho la Biashara ndogo na za Kati nchini Uganda.
Wito huo umetolewa wakati nchi hiyo inakaribia kuwa na mafuta yake ya kwanza licha ya kuchelewa kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Serikali ilitabiri kuwa nchi hiyo itakuwa na mafuta yake ya kwanza mwaka 2016.Hata hivyo kumekuwa na ucheleweshaji na kuahirishwa kwa muda kuafikiwa hilo.
Mkurugenzi wa Shirikisho la biashara ndogo na za kati ,Bw John Walugembe, amesema biashara zinafaa kukisia matarajio yao katika sekta ya mafuta na gesi na kujizuia kuomba mikopo.
Waganda waliowekeza katika sekta ya mafuta na gesi miaka kadhaa iliyopita wamekuwa wakikadiria hasara na bado hawana uhakika ni lini uzalishaji utaanza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |