Serikali ya Tanzania inakusudia kufungua mashamba makubwa ya mazao ya kimkakati ikiwamo korosho lengo kukabiliana na nchi washindani katika nyanja za uzalishaji, ubora na bei ya bidhaa zitokanazo na mazao hayo kwenye soko la dunia.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo, Nyasebwa Chimagu, aliyasema hayo jana wilayani Manyoni wakati wa mafunzo ya kilimo bora cha korosho ambayo yanatolewa na wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), Kituo cha Naliendele kwa wakulima wa korosho wa Halmashauri za Manyoni na Itigi mkoani Singida.
Alisema serikali imedhamiria uzalishaji wa mazao ya kimkakati kama korosho ili iweze kuhimili ushindani kwenye soko la dunia.
Alisema ili kufikia azma hiyo, Tanzania imedhamiria kuongeza uzalishaji wa korosho kutoka tani 300,000 zinazozalishwa hivi sasa hadi tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2025.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |