Baada ya majuma kadhaa ya kusubiri, mabingwa mara 13 wa Ligi Kuu ya Kenya, AFC Leopards sasa wanatarajiwa kutambulisha wanasoka wapya walioingia kambini mwao msimu huu kwa mashabiki wiki ijayo. Mwenyekiti wa Klabu hiyo Dan Shikanda, ambaye amekataa kufichua majina ya wachezaji wapya waliowasajili hadi kufikia sasa, amesisitiza kwamba wamesajili wachezaji watano pekee walioridhisha vinara wa benchi ya kiufundi. Mbali na fowadi Harrison Mwendwa wa Kariobangi Sharks, wachezaji wengine ambao waliwahi kuhusishwa na uwezekano mkubwa wa kusajiliwa na Leopards ni mshambuliaji wa zamani wa Kakamega Homeboyz, Peter Thiong'o na Fabrice Mugheni ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo). Shikanda pia amesema, kocha wa sasa wa timu hiyo Anthony Kimani, ambaye aliongoza Leopards kupata matokeo ya kuridhisha katika msimu wa 2019-20, ataendelea kukinoa kikosi hicho.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |