• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapato yatokanayo na zao la pamba kuongezeka Uganda

    (GMT+08:00) 2020-10-09 18:23:29

    Mapato yatokanayo na mauzo ya pamba nje ya nchi nchini Uganda yanatarajiwa kuongezeka kufuatia kuzinduliwa kwa shirika la maendeleo ya pamba nchini humo. Shirika hilo litasaidia kupunguza uchelewishwaji wa vyeti vinavyohitajika katika usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi kutoka kwa serikali.Hatua hiyo itapelekea Uganda kusafirisha idadi kubwa ya pamba nje ya nchi hivyo kuongeza mapato kwa nchi kupitia zao hilo.Takwimu zinaonesha kuwa pamba ni miongoni mwa bidhaa 10 zinazosafirishwa kwa wingi nje ya nchi ambapo katika mwaka wa fedha wa 2018 na 2019, zao la pamba liliingizia nchi jumla ya dola za kimarekani milioni 54.26. Hata hivyo mapato hayo yalipungua hadi dola milioni 41.69 katika mwaka wa fedha wa 2019 na 2020. Uganda imesema mbali na utaratibu mrefu wa kutoa vyeti vinavyohitajika katika kusafirisha bidhaa nje, kupungua kwa mapato hayo pia kulichangiwa na janga la corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako