• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miundombinu bora yapunguza gharama usafirishaji

    (GMT+08:00) 2020-10-09 18:23:46

    Wakulima wa tumbaku mkoani Mbeya nchini Tanzania wamesema uboreshaji wa miundombinu ya barabara wilayani Chunya umeanza kupunguza gharama za uzalishaji wa zao hilo na sasa gharama za usafirishaji wa pembejeo zimepungua.

    Wakulima wa maeneo ya Mtande na Matwiga wamesema awali walikuwa wanachelewa kupata pembejeo hasa mbolea na wanapozipata walikuwa wakiuziwa kwa gharama kubwa.

    Kaul;i hiyo ya wakulima inakuja miezi michache tu baada ya kuboreshwa kwa barabara ya kutoka Mbeya kwenda Makongorosi.

    Zamani wakulima hao walikuwa wanachukulia mbolea Mbeya Mjini, lakini sasa wanapelekewa mpaka katika maeneo ya vijiji vyao kupitia vyama vya ushirika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako