Jukwaa la Kiuchumi Duniani WEF, limeahirishwa hadi mwezi Mei, 2021 na limepangwa kufanyika kwenye mji wa Lucerne karibu na Bürgenstock. Mkutano huo uliahirishwa kutokana na janga la virusi vya corona.
Mkurugenzi Mkuu wa jukwaa hilo, Adrian Monck alisema mkutano huo utafanyika kwa kuzingatia masharti yote yaliyowekwa ya afya na usalama wa washiriki pamoja na mwenyeji wa mkutano huo.
Monck alisema mkutano huo utaangazia zaidi suluhisho linalohitajika kuzishughulikia changamoto kubwa zaidi duniani.
Hata hivyo,mkutano mwengine wa kilele kwa njia ya video ulipangwa kufanyika Januari 25. Mkutano wa ana kwa ana kwa kawaida huwashirikisha viongozi wa serikali,viongozi wa kibiashara, taasisi mbalimbali, wanaharakati na watunga sera.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |