• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TANZANIA: WAFUGAJI WAAGIZWA KUOGESHA MIFUGO WAO.

    (GMT+08:00) 2020-10-12 17:35:04

    Wizara ya Mifugo na Uvubi imewaagiza wafugaji kuhakikisha wanaogesha mifugo yao ili kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na kupe, ambayo huchangia vifo vya ng'ombe nchini Tanzania kwa asilimia 72.

    Katibu mkuu katika wizara hiyo, Prof. Elisante Ole Gabriel, alitoa agizo hilo jana,alipokuwa akizindua awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo nchini, ilyofanytika katika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.

    Alibainisha kuwa katika vfo hivyo, asilimia 44 huchangiwa na ugonjwa wa ndigana kali. Aidha aliongeza kwa kusema kuwa hasara itokanayo na magonjwa hayo inakadiriwa kuwa takriban shilingi bilioni 145, na kusababusha kupungua uzalishaji maziwa, nyama kutokana na kukonda, kushuka kwa thamani ya ngozi, kupoteza wanyama kazi na udumavu wa ndama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako