Janga la corona litawasukuma watu milioni 100 kwenye lindi la umaskini ifikapo mwaka ujao. Imesema ripoti ya uchunguzi ya Benki ya Dunia. Eneo litakaloathirika zaidi ni bara la Afrika .
Ripoti hiyo inasema kwamba janga la corona na uvamizi wa nzige wa jangwani walioathiri mataifa ya Afrika Mashariki na kutishaia uhaba wa chakula, kupoteza ajira na biahsara kuathiriwa ni sababu kuu zitazowasukuma watu wengi barani Afrika kwenye umaskini.
Eneo la Afrika Mashariki limepoteza kati ya shilingi trilioni 4 na trilioni 8.5 mwaka huu pekee kutokana na majanga haya. Sekta zilizoathirika vibaya na janga la corona ni utalii, ambako maelfu ya watu walipoteza ajira.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |