MADEREVA wa matrela wanaosafirisha bidhaa katika nchi za Uganda na Rwanda, wamemlaumu vikali Waziri wa Uchukuzi James Macharia kwa kukosa kushughulikia tatizo la msongamano katika mpaka wa Malaba.
Msongamano huo unakisiwa kufikia umbali wa kilomita 80.
madereva hao walimkashifu vikali Bw Macharia kwa kutozuru eneo hilo tangu janga la Covid-19 kutua nchini mwezi Machi.
Bw Mathews ambaye husafirisha vyuma kutoka Mombasa hadi mjini Fort Portal, Uganda, amesema madereva wa kusafirisha bidhaa wamekuwa wakiteseka sana tangu janga la Covid-19 kutua nchini.
Msongamano huu umeletwa na maafisa wa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru (KRA) mpakani. Ajali nyingi zimetokea kwa sababu tu ya hali hii.
Dereva mwingine Mohamed Shukri alisisitiza kuwa wanataka kukutana na mawaziri wa uchukuzi wa nchi hizo mbili za Kenya na Uganda ili kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu mkwamo huo.
Alilalamika kwamba takriban madereva 4,000 wamekwama eneo hilo kwa sababu ya kujikokota kwa maafisa wa Uganda kuwapa matokeo ya vipimo vya virusi vya corona, ambavyo ndivyo vinasababisha Covid-19.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |