Waziri wa Kilimo wa Ethiopia, Oumer Hussien, amesema ndege zaidi za kunyunyiza dawa zitapelekwa kukabiliana na makundi ya nzige wanaovamia mashamba nchini humo.
Hii ni baada ya ndege za kupuliza dawa kuanguka mapema mwezi Oktoba na kurudisha nyuma jitihada za kupambana na wadudu hao waharibifu.
Waziri amesema nzige katika maeneo manne wamepulizwa dawa kwasababu wamekuwa tishio kwa usalama wa chakula nchini Ethiopia.
Amesema Wizara inaendeleza mchakato wa kubaini mashamba yaliyoathiriwa zaidi na uvamizi wa nzige ili kuwapa usaidizi wenye mashamba hayo.
Nzige walionekana katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki ambako wamesababisha uharibifu wa mimea.
Wataalamu wametaja uvamizi wa sasa wa nzige kuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 60.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |