Matumaini ya kiungo Paul Pogba kwenda kujiunga na Real Madrid huenda yakashindwa kutimia baada ya miamba hiyo ya Satiago Bernabeu kuwafikiria wachezaji tofauti katika mpango wa kuunda Galacticos mpya. Mabingwa hao wa La Liga wanatunza pesa zao kwa ajili ya kufanya usajili mkubwa kwenye dirisha la majira ya joto mwakani, huku wachezaji wanaotaka kuwasajili ni Kylian Mbappe, Erling Haaland na kiungo kinda Eduardo Amavinga. Pogba, 27, hakutaka kuweka siri kuhusu kutamani maisha ya kwenda kucheza Bernabeu. Lakini, gazeti la AS linaandika kwamba Pogba anaweza kubaki kwenye huzuni kubwa. Mbappe anaendelea kubaki kwenye rada za Los Blancos baada ya kuonyesha dhamira ya kuachana na Paris Saint-Germain mwakani wakati huo mkataba wake ukiwa umebaki mwaka mmoja. Ripoti kutoka Hispania zinadai kwamba PSG wanaweza kumuuza Mbappe kwa bei ndogo kati ya Pauni 111 milioni na Pauni 91 milioni wakati atakapoingia miezi yake 12 ya mwisho ya mkataba wake huko Paris.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |