• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya Benki ya KCB Kenya imepokea Sh16.2bilioni kwa ajili ya mikopo kwa wafanyabiashara wadogo, na wa kati

    (GMT+08:00) 2020-10-14 20:16:01

    Benki ya KCB Kenya imepokea Sh16.2bilioni ($ 150 milioni), kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kusaidia ukuaji wa jalada endelevu la Fedha ya mabadiliko ya anga ili kusukuma juu mikopo kwa wafanyabiashara wadogo, na wa kati pamoja na biashara zinazomilikiwa na wanawake.

    Njia ya mkopo itachangia ukuaji wa uchumi wa Kenya kwa kusaidia kukuza mikopo na kutengeneza nafasi za ajira, haswa kwa wanawake.

    Benki ya biashara KCB imeingiza uendelevu wa mazingira katika mkakati wake, katika maeneo yote ya biashara.

    Mkurungenzi mkuu wa KCB Oigara amesema wanafuraha kushirikiana na IFC katika chombo hiki cha kifedha cha ubunifu, ambacho kitatuwezesha kufufua uchumi wakati nchi huu nchi imeanza kurudi kwa hali yake ya kawaida kutokana na athari za COVID-19. Aidha amesema Itatuwezesha kufungua njia ya kupata mikopo zaidi kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako