Wakulima ambao wanafanya kilimo kikubwa chini ya "shina moja" wanatarajia kupata shilingi mia tatu kwa kilo ya matunda wanapeleka kwenye kiwanda chao.
Wakizungumza wakati wa mkutano kwenye shamba huko Mathira, wakulima hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Patrick Muchiri wanasema kuwa chini ya mfumo huo, watazalisha mazao bora ambayo itatoa kahawa bora ulimwenguni.
Wakulima ambao wana mipango ya kuanzisha kiwanda kidogo kwa bidhaa yao iliyosindikwa wanasema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakinyonywa na wasagaji na wauzaji ambao wanashirikiana kuamua malipo yao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |