Licha ya corona kulemeza biashara na uchumi katika nchi nyingi za Afrika sekta ya huduma ili nawiri dhidi ya janga la corona na kuandikisha mapato ya kuvutia katika miezi mitatu iliyopita.
Kulingana na Ripoti ya Utendaji ya Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA) kwa kipindi cha Julai hadi Septemba - robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2020/21 - inaonyesha kwamba asilimia 75 ya mapato yalikusanywa kutoka kwa sekta tano kati ya 21 za uchumi.
Sekta tano za uchumi ni pamoja na: sekta ya mauzo ya jumla na rejareja ambayo inachangia asilimia 30 kwa kitita cha mapato, sekta ya utengenezaji ilishika nafasi ya pili na mchango wa asilimia 23.
Sekta ya habari na mawasiliano ilikuja ya tatu, ikichangia asilimia 9 ya mapato kwa hazina ya kitaifa.
Kulikuwa na ukuaji wa mapato katika baadhi ya sekta muhimu kama vile viwanda ambayo ilikua kwa asilimia 18, habari na mawasiliano ilikua kwa asilimia 20, wakati mapato kutoka kwa sekta ya mauzo ua jumla yalikua kwa asilimia 2.3.
Ripoti ya utendaji wa mapato pia ilionyesha kupungua kwa mapato yaliyosajiliwa katika sekta kama vile malazi na huduma za chakula, ikipungua kwa asilimia 58. Sekta nyingine iliyoathirika sana ni elimu ambapo ukuaji wa mapato ulipungua kwa asilimia 31.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |