• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Serikali yaeleza kwa nini bei za chakula zimeongezeka

    (GMT+08:00) 2020-10-15 18:21:11

    Bei za bidhaa nyingi za chakula ambazo zimepanda katika siku za hivi karibuni nchini Rwanda zinatarajiwa kushuka siku chache zijazo,wakati wakulima wakianza kuvuna.

    Bei za bidhaa za chakula kama vile viazi,mchele,maharage,na nyanya nchini Rwanda zimekuwa zikiongezeka na kusababisha wasiwasi kuhusu utoshelevu wa chakula nchini humo.

    Wizara ya Biashara na Viwanda hata hivyo imesema kuwa hali hiyo haikusababishwa na changamoto za uzalishaji lakini ni mtindo wa msimu kufuatia kuisha kwa hifadhi kutoka mavuno ya msimu uliopita.

    Waziri wa Biashar na Viwanda nchini humo, Soraya Hakuziyaremye, amesema kuwa kwa baadhi ya mazao,wakulima wanatarajiwa kuanza kuvuna wiki chache zijazo,jambao ambalo litasababisha bei za bidhaa kupungua na kuwa imara kwa muda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako