Uganda ni miongoni mwa nchi chache ambazo zimeendelea kufanya vizuri kiuchumi duniani licha ya janga la Covid 19 ambalo limeendelea kuyumbisha dunia. Waziri wa fedha wa Uganda Bw David Bahati amesema uchumi wa Uganda umeendelea kukua kwa asilimia 3. Bahati ameongeza kuwa uchumi wa nchi nyingi duniani umeendelea kushuka ikiwemo Marekani. Ameongeza kuwa baadhi ya sekta ambazo zimeathiriwa ni pamoja na sekta ya utalii lakini hata hivyo sekta ya kilimo imeendelea kufanya vizuri licha ya janga la corona kuendelea kote duniani. Amesema serikali ya Uganda imewekeza jumla ya shilingi trilioni 1 katika benki ya maendeleo ya Uganda ili iweze kutoa mikopo na kuchangia katika maendeleo ya sekta mbali mbali nchini humo. Amesema serikali imeitaka benki hiyo kutoa mikopo kwa riba ya chini na watu kuanza kulipa mkopo huo baada ya mwaka mmoja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |