• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TCRA yawataka vijana kukumbatia uchumi wa kidigitali

    (GMT+08:00) 2020-10-16 16:45:35

    Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Asajile John, amewataka vijana nchini Tanzania kutumia vyema teknolojia za mawasiliano hususani TEHAMA katika shughuli za uzalishaji, ili kulisaidia taifa kufikia uchumi wa kidigitali.

    Asajile alitoa rai hiyo juzi wakati wa kongamano lilowahusisha vijana wa shule za sekondari na vyuo kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya kwenye Siku ya Kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, lililoandaliwa na Shirika la Lightness Tanzania.

    Alisema vijana wanapaswa kuenzi falsafa ya Hayati Mwalimu Nyerere ya kujitegemea kwa kuhakikisha wanatumia teknolojia za mawasiliano kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutumia kwenye shughuli za biashara, kilimo na wanafunzi kujisomea na kutafuta ajira.

    Aidha Asajile alisema lengo la TCRA ni kuhamasisha vijana kutumia kwa manufaa yao kama vile kufahamu mabadiliko mbalimbali yanatokea duniani na kuwa makini na matumizi ya TEHAMA ili kujiepusha na uvunjifu wa sheria za mitandao.

    Alisema falsafa ya uhuru wa kujitegemea kama ajenda yao katika kumuenzi Mwalimu Nyerere, inawakumbusha vijana kujiamini, kuwa wabunifu na kufanya utafiti ili ulete tija kwa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako