Mapadre wawili wa Kanisa Katoliki mapema wiki hii walifikishwa mahakamani mjini Vatcan kwa madai ya unyanyasaji wa kingono. Kasisi wa kwanza kwa jina Gabriele Martinelli, aliye na umri wa mika 28, anashutumiwa kumnyanyasa kingono mvulana aliyekuwa akitumikia kwenye madhabahu ya kanisa kati ya mwaka 2007 na 2012.
Mwingine ni Padre Enrico Radice, mwenye umri wa miaka 72, ambaye anashtakiwa kwa kuficha madai ya unyanyasaji huo wakati alipokuwa mkuu wa shule ya theolojia ambako tukio hilo linadaiwa kufanyika.
Huku makasisi kadhaa wamekwisha kabiliwa na mashitaka kote duniani, Vatcan haijawahi kuendesha kesi inayohusiana na unyanyasaji wa kingono katika mahakama yake. Hao ndio makasisi wa kwanza kuwahi kushtakiwa katika mji huo wa Vatican
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |