• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasomi na vyombo vya habari vya Afrika wakanusha shutuma za udukuzi wa China barani Afrika

    (GMT+08:00) 2020-10-19 18:40:01

    Mwezi Mei mwaka huu, jopo la washauri bingwa la Marekani Heritage Foundation lilitoa ripoti ya kuishutumu China kufanya udukuzi katika majengo ya serikali za nchi za Afrika yaliyojengwa au kukarabatiwa na kampuni za China. Hivi karibuni katika kipindi cha kuadhimisha miaka 20 ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, ripoti hiyo ya uongo imeanza kuenezwa tena na baadhi ya vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii, ili kuharibu uhusiano na ushirikiano mzuri kati ya China na Afrika.

    Hivi karibuni vyombo vya habari vya nchi mbalimbali za Afrika vimetoa tahariri vikifichua unafiki wa nchi za magharibi ambazo hazitaki kuisaidia Afrika kupata maendeleo. Oktoba 12 Gazeti la The Authority la Nigeria lilitoa tahariri yenye kichwa cha "ripoti ya uongo ya Heritage Foundation ni hadithi ya kutungwa isiyo na msingi", ikiikosoa ripoti hiyo kuwa haina ushahidi wowote wa kuaminika, na kusema Marekani inajifanya Mwokozi wa Dunia na kuitaka Afrika eti "ijiepushe na hatari zinazotokana na China", ili kufikia lengo lake la kulinda maslahi yake ya kiuchumi na kisiasa barani Afrika. Tahariri hiyo inaona Marekani inajaribu kuharibu uhusiano na ushirikiano kati ya China na Afrika kwa kutumia upendeleo wa kiitikadi.

    Mtafiti wa Chuo cha Sayansi ya Siasa na Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo kikuu cha Abuja nchini Nigeria Bw. Ibrahim, Ijumaa iliyopita alitoa makala kuhusu mustakbali wa uhusiano kati ya China na Afrika kwenye vyombo vya habari vya Ghana, akikanusha shutuma za udukuzi wa China barani Afrika, na kusisitiza kuwa kueneza kauli za chuki dhidi ya China kunaweza kuimarisha hata zaidi ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Siku hiyohiyo, Gazeti la Gold Street Business la Ghana lilitoa tahariri ikisema shutuma zilizotolewa na Marekani kuhusu China kufanya udukuzi barani Afrika hazina msingi wowote, na uhalisia ni kwamba katika muda mrefu uliopita ni nchi za magharibi ndizo zilizoendelea kudukua serikali za nchi za Afrika, ili kuimarisha ushawishi wake katika bara la Afrika na hata dunia nzima.

    Makala hiyo inasema Afrika ina haki ya kuchagua mwenzi wa ushirikiano, na imeichagua kwa busara China kuwa mwenzi na rafiki yake. Makala hiyo inaongeza kuwa misaada ya China kwa Afrika haina masharti ya kisiasa, na katika miaka ya hivi karibuni, China imezisaidia nchi za Afrika kupambana na milipuko ya Ebola na virusi vya Corona, hatua ambazo zimeonyesha wazi urafiki kati ya pande hizo mbili. Tahariri hiyo inasisitiza kuwa kusambaza kauli za chuki dhidi ya China kunaweza tu kuzidisha uhusiano na ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako