Kampuni za Wachina, zilizo na karibu miradi 1,564 ambayo ilikuwa ikifanya kazi katika miongo miwili iliyopita, ndio washiriki wakuu katika mazingira ya uwekezaji wa Ethiopia afisa wa Tume ya Uwekezaji ya Ethiopia ( EIC) amesema.
Mekonen Hailu, Mkurugenzi wa Mawasiliano katika EIC, amesema kampuni za Wachina zinawekeza katika sekta za aina nyingi za uchumi nchini Ethiopia na wamejitolea kwa uwekezaji wa muda mrefu.
Kulingana na takwimu kutoka Tume ya Uwekezaji ya Ethiopia (EIC), kampuni za Wachina zimetekeleza karibu miradi 1,564 ya uwekezaji ambayo imefanya kazi sasa kwa miongo miwili iliyopita, kutoka 1998 hadi Machi 2020.
Kati ya miradi 1,564, miradi 1,133 inahusika katika sekta ya utengenezaji, ambayo ni eneo kuu la uwekezaji wa kipaumbele na serikali ya Ethiopia, kulingana na Mekonen.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |