• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • John Bocco apumzishwa zaidi kutoka timu ya taifa ya Tanzania kutokana na majeruhi

    (GMT+08:00) 2020-10-20 17:33:55

    Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Etienne Ndayiragije, amemuondoa kikosini mshambuliaji John Bocco kutokana na hali yake kiafya kutoimarika. John Bocco aliitwa katika kikosi hicho akiwa ametoka katika majeraha aliyopata wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ilipocheza na Mtibwa Sugar, Septemba 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Bw. Ndayiragije amesema maandalizi yanaendelea vizuri na wachezaji wote wamewasili kambini, lakini Bocco ameonekana hayuko vizuri na amemruhusu aendenlee na matibabu. Amesema kukosekana kwa mchezaji huyo ni pengo, lakini wapo wengine watapata nafasi akiamini wataitendea haki nafasi hiyo. Taifa Stars inajiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi, na kocha huyo amesema Burundi ni kipimo kizuri kwao kuelekea mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Tunisia, kwa sababu soka wanalocheza linafanana na Tunisia. Katika hatua nyingine, winga wa Taifa Stars, Simon Msuva na beki Nickson Kibabage, wanaochezea Difaa El Jadid ya Morocco, wamewasili jana na kujiunga na wenzao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako