WAKUZAJI miraa nchini wameeleza wasiwasi kwamba huenda wakapoteza soko la Somalia kabisa, baada ya Ethiopia kuanza kusafirisha zao hilo nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, shirika la ndege la Ethiopia, liliwasilisha shehena ya kwanza ya zao hilo katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Aden Adde, Mogadishu.
Hali hiyo imezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wakuzaji hao nchini, ikizingatiwa ndio wamekuwa wakidhibiti mauzo ya zao Somalia kwa muda mrefu.
Wakenya walishindwa kupenya soko hilo kutokana na kiwango cha juu cha kodi.
Vyombo hivyo viliripoti kwamba serikali ya Somalia imeiruhusu Ethiopia kuendesha biashara hiyo nchini humo, huku marufuku dhidi ya Kenya ikiendelea kuwepo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wakuzaji Miraa cha Nyambene (Nyamita), Bw Kimathi Munjuri, alisema kuwa serikali ya Somalia pia imeimarisha usalama katika Bara Hindi kuhakikisha hakuna miraa kutoka Kenya inaingizwa nchini humo.
Bw Munjuri aliiomba serikali ya Kenya kufanya mazungumzo na Somalia ili kuwarejeshea udhibiti wa soko hilo.
wakulima sasa wamechoshwa na mkwamo huo ambao umedumu kwa miezi saba hadi wengi wao wanakumbwa na matatizo ya kifedha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |