• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki kuu za Kenya kutokana na janga la corona zimetengeneza faida ya chini

    (GMT+08:00) 2020-10-20 19:20:42

    Benki kuu za Kenya kutokana na janga la corona zimetengeneza faida ya chini mno kando na ile walitarajia.

    Idadi ya wanaochukua mkopo imeenda chini pia na kuongezeka kwa kiwango cha mikopo mibaya, kuashiria kupunguzwa kwa gawio kwa wanahisa.

    Kulingana na ripoti maalum ya wakala wa Fitch kwenye benki nane ambazo zinadhibiti asilimia 83 ya amana za tasnia na asilimia 76 ya mali yote, hali dhaifu za utendaji zimesababisha mapato ya chini na faida kwa wakopeshaji.

    Hali hiyo imechangiwa na uvamizi mkubwa wa nzige tangu Julai 2019 ambayo inaweza kusababisha shinikizo zaidi kwa ubora wa mali ya benki kupitia kukopesha wakulima wadogo na jamii za wakulima.

    Fitch, kupitia ripoti yake iliyopewa jina la " Coronavirus Impact on Large Kenyan Banks'" inaonyesha kuwa mapato ya wastani katika benki hizi kubwa ulipungua kwa alama 730 za msingi (bp) hadi asilimia 11.6 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako