• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Maendeleo wa Afrika (ADF) imeidhinisha mkopo($ 50.7 milioni) kwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2020-10-20 19:21:02

    Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Maendeleo wa Afrika (ADF) imeidhinisha mkopo wa UA milioni 36 ($ 50.7 milioni) kwa Tanzania, kufadhili jibu la taifa kwa janga la COVID-19.

    Mkopo huo, kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (CRF), kwa ajili ya corona itasaidia Serikali ya Tanzania Dola milioni 109, kuweza kuweka mikakati ya kupambana na corona.

    Mpango huo unakusudia kujenga uimara wa uchumi, wakati unapunguza athari za kijamii na kiuchumi na kiafya za janga la COVID-19, haswa kwa wafanyabiashara wa ndani, wakazi wenye wako katika mazingira magumu na mfumo wa afya wa nchi.

    Janga hilo limeongeza shinikizo kwa vituo vya afya vya Tanzania, mifumo ya ulinzi wa jamii na imepunguza ukuaji wa makadirio ya nchi hiyo zaidi ya 6.2% - wastani kwa miaka mitano iliyopita, na ambayo ilikuwa imeifanya kuwa moja ya watendaji bora katika Afrika Mashariki. Ukuaji sasa unakadiriwa kupungua kutoka kwa makadirio ya kabla ya COVID ya 6.4% hadi kati ya 3.6% na 2.6%.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako