Kampuni kadhaa za kusaga unga Magharibi mwa Kenya, zinakabiliwa na hatari ya kufunga biashara zao baada ya wanunuzi wengi wa unga kuacha kununua bidhaa hiyo na kuamua kutumia unga unaosagwa katika vinu vya kawaida, wanaoamini kuwa salama.
Watu wengi wanahofia unga unaosagwa viwandani una sumu ya aflatoxin kutokana na kiwango ambacho serikali ya Kenya imetoa kizingatiwe.
Hii ina maana kuwa baadhi ya wafanyakazi katika kampuni hizi watapoteza ajira.
Kampuni 10 ndogo ndogo za usagaji tayari zimewatuma baadhi ya wafanyakazi wao katika likizo ya lazima, kutokana na ukosefu wa soko kwa bidhaa zao. Wanasema mahindi mengi yanayozalishwa nchini yana kiwango cha aflatoxin kinachopelekea mazao hayo kutochukuliwa kuwa salama kwa matumizi ya binadamu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |