Nchi za pembe ya Afrika zinakabiliwa na uvamizi wa nzige wa jangwani, ambapo makundi mapya ya nzige yanatarajiwa kuvamia nchi za Ethiopia na Somalia wiki chache zijazo.
Kwa mujibu wa shirika la Chakula Ulimwenguni (FAO), limebainisha kuwa uvamisi wa nzige hao pia utaikumba nchi ya Kenya.
Eeno la pembe ya Afrika inatishiwa na uvamizi mbaya wa nzige wa jangwani baada ya ule wa miaka 70 iliyopita, ambapo mabilioni ya nzige ambao walivamia kanda hii mwaka huu, wakiharibu makumi ya maelfu ya hekta za mazao, wamezaliana tena.
Nzige wa kike hutaga mayai zaidi ya 100 kwa wastani, hivyo watoto wanaotoka kwenye mayai hayo wanaweza kuongezeka mara 20 kila miezi mitatu..
Watoto wa nzige waliozaliwa hivi karibuni wamefikia hatua ya kukomaa kwa kuanza kuruka, sasa yanaunda makundi mapya ya kubamia mashamba, ambapo tayari wameonekana nchini Yemen na Kaskazini mashariki mwa Ethiopia.
Mwishoni mwa mwezi Oktoba, watakuwa wamevamia Ethiopia mashariki na Somalia ya kati, halafu, kaskazini mwa Kenya itakumbwa tena mnamo mwezi Novemba.
Wimbi hili jipya linatokana na upepo mkali kutoka Yemen ambao ulienea juu ya Pembe la Afrika, ukibeba mawingu makubwa meusi ya mabilioni ya nzige wa jangwani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |