• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kushiriki michezo ya CECAFA ya kufuzu AFCON kwa Chipukizi wa U-17, U-20

    (GMT+08:00) 2020-10-21 18:34:25

    Nchi 10 zimethibitisha kushiriki mechi za Shirikisho la vyama vya Soka vya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) 2021 kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 na 20. Taarifa ya Kamati Kuu ya Cecafa imesema mechi za kufuzu kwa fainali za AFCON U-20 zimeratibiwa kuchezwa kati ya Novemba 22 na Disemba 6 nchini Tanzania, huku zile za U-17 zikipangiwa kuchezwa kati ya Disemba 13-28 nchini Rwanda.

    Kwa kila kitengo, timu hizo zitapangwa kwa makundi mawili ambapo vikosi viwili vya kwanza vitafuzu moja kwa moja kushiriki nusu-fainali. Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa), Regis Uwayezu, amethibitisha kwamba Rwanda haitashiriki mchujo wa kufuzu kwa fainali za AFCON U-20 mwaka huu. Waandaaji wa mashindano hayo ya CECAFA wanatarajiwa kuandaa droo ya mechi za makundi wiki ijayo mjini Arusha, Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako