• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VPL: Simba kuwa na wakati mgumu mjini Sumbawanga

    (GMT+08:00) 2020-10-21 18:35:23

    Timu ya Simba kimeondoka jana kwenda mjini Sumbawanga, kuifuata Tanzania Prisons, huku Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck, akisema amejipanga kukabiliana na kila changamoto ili kurejea na ushindi. Simba imeondoka wameondoka na kikosi cha nyota 22, wakitarajia kukutana na Prisons keshokutwa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Mandela. Wachezaji waliokosekana katika safari hiyo, ni nahodha John Bocco, Gerson Fraga wanaouguza majeraha, Clatous Chama na Pascal Wawa walisafiri. Simba imekwenda Sumbawanga ikiwa imejirisha katika maandalizi baada ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege na kushinda mabao 3-1 wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Sven alisema anafahamu aina ya mchezo anaokwenda kukutana nao ni mgumu kutokana na soka wanalocheza Prisons. Sven alisema Prisons ni timu ngumu na inacheza soka la kutumia nguvu, hivyo kumfanya akiandae kikosi chake kwa mbinu nyingi na kuwaweka wachezaji tifi zaidi."Prisons nawajua wanacheza soka la nguvu, lakini matumaini ya sisi kufanya vizuri ni makubwa kutokana na kikosi cha wachezaji 22 nilichoondoka nacho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako