Tamasha la tano la vijana wa China na Afrika limefunguliwa jana hapa Beijing. Kauli mbiu ya tamasha hilo la siku 7 ni "Kuunganisha ndoto za vijana na kufungua kwa pamoja zama mpya ya uhusiano kati ya China na Afrika", ambapo wajumbe 42 wa vijana wa Afrika nchini China watafanya ziara mjini Beijing na mkoani Jiangxi, kutembelea idara za serikali, kampuni, maeneo ya sayansi na teknolojia, kuhudhuria kongamano la vijana wa China na Afrika, na kutembelea vivutio vya utamaduni na mandhari ya asili.
Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Deng Li, amewataka vijana wa China na Afrika waendelee na mshikamano na ushirikiano, na kutoa msukumo mpya kwa maendeleo endelevu ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |