Wenyeji RS Berkane wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Pyramids ya Misri kwenye mchezo wa fainali uliofanyika Uwanja wa Prince Moulay Abdallah Jijini Rabat, Morocco. Bao hilo la pekee lilifungwa na Mohssine Iajour dakika ya 15 tu ya mchezo huo, na kuiwezesha RS Berkane kuiangusha timu ya Misri, Pyramids na kutwaa taji lao la kwanza kabisa la Kombe la Shirikisho wakicheza fainali ya michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo. Michuano ya mwaka huu ilichelewa kumalizika baada ya kusimama tangu katikati ya Machi, ikiwa katika hatua ya Nusu Fainali kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |