• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huduma za biashara ya kielektroniki za China zaenea kwenye tarafa 832 zilizoko nyuma kiuchumi nchini

    (GMT+08:00) 2020-10-27 16:51:47

    Huduma za biashara ya kielektroniki za China zimeenea katika tarafa 832 zilizoko nyuma kiuchumi kote nchini, na thamani ya mauzo ya rejareja kwenye mtandao wa Internet katika maeneo ya vijijini imeongezeka kutoka dola za kimarekani milioni 2.7 ya mwaka 2014, na kufikia dola za kimarekani bilioni 253 mwaka 2019.

    Hivi sasa, kiwango cha upatikanaji wa huduma za biashara ya kielektroniki kwenye vijiji vilivyoko nyuma kiuchumi nchini China kimeongezeka kutoka chini ya asilimia 70 hadi kufikia asilimia 98. Pia kiwango cha matumizi ya mtandao wa Internet kwenye shule za msingi na za sekondari kimeongezeka kutoka asilimia 79.2 ya mwishoni mwa mwaka 2016, kufikia asilimia 98.7 ya mwezi Agosti mwaka 2020. Huduma za matibabu kupitia mtandao wa Internet Telemedicine zimeenea kwenye hospitali za ngazi za taifa na wilaya zilizoko nyuma kiuchumi, na utoaji wa msaada wa kupunguza umaskini kupitia mtandao wa Internet unatarajiwa kuwanufaisha watu wengi zaidi wenye matatizo ya kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako